.

.

.

.


TUMSIFU THE GREAT

BEHIND THE SCENE

  • MOVIE SHOOTING

    Wakati wa utengenezaji wa movie inayoitwa BACK TO SCHOOL
  • BACK TO SCHOOL

    SHOT IN TANGA TANZANIA
  • MUSIC VIDEO

    Wakati wa utengenezaji wa music video inakwenda kwa jina la I NEED U
  • MOVIE BACK TO SCHOOL

    Directed by TUMSIFU KOMBE
  • BACK TO SCHOOL

    wakati wa utrngenezaji wa movie inayoitwa BACK TO SCHOOL
  • MOVIE NAME-WIVU

    Behind the scene ya upigaji picha wa movie inayoitwa WIVU
  • MUSIC VIDEO HERE

    Upigaji wa picha wa Music video, msanii anajulikana kwa jina la Rider, wimbo DECEMBER, Shot in Tanga Tanzania
  • MOVIE-WIVU HERE

    Upigaji picha wa movie inayojulikana kwa jina la WIVU

Showing posts with label BUSSINESS NEWS. Show all posts
Showing posts with label BUSSINESS NEWS. Show all posts

Tuesday, April 30, 2013

DVD YA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA SASA INAPATIKANA

www.rutaalicia.blogspot.com
DVD hii itakupa mwangaza ni jinsi gani unaweza kuendesha maisha yako bila ya kutegemea ajira za serikali,utajifunza kila kitu kuhusu ujasiriamali,kuanzisha kampuni,kutunza kumbukumbu za kibiashara na zaidi ya yote ni jinsi gani unaweza kutumia mtandao kujipatia kipato(how to make money on line).KWA WATAKAOHITAJI TAFADHALI WASILIANA NA NAMBA 0714101838/ 0752346930/ 0718213540/ 0765171745 AU KWA BARUA PEPE aliciarutajumbukilwa@gmail.com

Monday, June 4, 2012

SEBASTIAN KOLOWA UNIVERSITY COLLEGE-KUTANGAZWA KWA ZABUNI


               SEBASTIAN  KOLOWA UNIVERSITY COLLEGE

                                                                 OF

                                     TUMAINI UNIVERSITY MAKUMIRA
                                                 P.O. BOX 370, Lushoto.

                                    Email: tumasosekuco@gmail.com


           ZABUNI YA KUENDESHA CAFTERIA YA WANACHUO
             KWA MWAKA 2012/2013

Sebastian Kolowa University College ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini University.Chuo hiki kipo umbali wa kilomita nane  kaskazini mwa mji wa Lushoto, Barabara kuu iendayo Mlalo , katika safu za milima ya kijani kibichi ya Usambala kwa jina la utani ; Uswisi  ya Afrika;
Chuo Kikuu kinakaribisha ZABUNI ya kuendesha Cafteria ya wanachuo. Cafteria hii inauwezo wa kuhudumia watu wasiopungua 600 kwa wakati mmoja.

Sifa za mwombaji;
(a) Awe na leseni ya kuendesha Cafteria/Hoteri/Mgahawa.
(b)            Awe na VAT na TIN. Aonyeshe uwezo wa kifedha
(c) Awe na uzoefu wa kuendesha Cafteria/Hoteri/Mgahawa kwa muda usiopungua miaka mitatu au zaidi.
(d)            Ataje kiwango cha kodi atakacholipa kwa mwezi. Cafteria inavifaa muhimu kama vile meza, viti,meza za maandalizi na vyumba baridi vya kuhifadhia vyakula mbalimbali.
(e) Ataje aina ya majiko atakayotumia Kwa kupikia kama vile Gesi Umeme au Mkaa.
(f)  Aainishe aina za vyakula na bei zake.
(g)Awe na vifaa vya msingi kama vile sahani, bakuli, glasi, vikombe, vijiko, umma, visu n.k.

MASHARTI YA ZABUNI;

(a)                        Maombi yaliyofungwa vizuri Kwa Lakiri na kuandikwa juu ya bahasha ‘ZABUNI YA KUENDESHA CAFTERIA YA WANACHUO’na kupelekwa kwa katibu, Serikali ya Wanachuo TUSO – SEKUCo, S.L.P 370, Lushoto.
(b)                        Mwombaji anatakiwa kulipa ada ya zabuni ya Tshs. 50,000/= (Elfu hamsini) tu, fedha ambayo hairudishwi.Zabuni iambatane na pay- in – slip ya malipo hayo, itakayolipwa kupitia, SEKUCo –SO. A/C No. 4162301220 NMB Lushoto Branch.
(c)Mwombaji ataruhusiwa kutembelea Cafteria hiyo siku za kazi kuanzia saa 2.30 asubuhi hadi saa10.30 jioni.
(d)                        Mzabuni atatakiwa kuonyesha aina ya vyakula na bei zake.
(e)Siku ya mwisho ya kuleta zabuni itakuwa tarehe 14 Julai 2012 saa 4.00 asubuhi.
(f)  Zabuni zitafunguliwa mbele ya wazabuni walioomba au wawakilishi wao kwenye ufunguzi huo tarehe 14 Julai 2012 saa 4.00 asubuhi.
(g)                        Muombaji atakayefanikiwa ataruhusiwa kuendesha Cafteria husika.

Kwa mawasiliano zaidi piga namba zifuatazo;

                    +255  7131  29097.
                     +255  7543  60761.
                     +255  7547  65515.

                             Katibu
SERIKALI YA WANACHUO  TUSO –SEKUCo
S . L . P 370, LUSHOTO.

Sunday, May 13, 2012

CHUO KIKUU SEBASTIAN KOLOWA UNIVERSITY COLLEGE CHATOA ELIMU YA URAIA VIJIJINI


Chuo kikuu kishiriki cha Tumaini university makumira, Sebastian Kolowa university College (SEKUco)kilichopo mkoani Tanga kimetoa elimu ya uraia kwa shule,na wananchi wilayani Lushoto.
    Sebastian Kolowa university College (SEKUco) ambacho ni chuo pekee Tanzania kinachotoa Shahada ya Elimu ya mahitaji maalumu, Shahada ya Sheria pamoja na Shahada na Eco-tourism na Nature Conservation kilitoa elimu hiyo jana 10/05/2012 kwa Kuanzia na Shule ya sekondari Magamba iliyopo wilayani Lushoto
      Kupitia  Organisation iliyoanzishwa Chuoni hapo na wanafunzi wanaosoma Elimu ya Siasa na Uongozi (political science and Public Adminstration) ijulikanayo kama SEPSSA ( Sekuco Political Science Student Association) walitoa elimu ya Uraia kwa Wanafunzi wa Shule hiyo kuhusiana na maswala ya haki na wajibu wa raia, uchaguzi huru na wa haki, na kujibu Maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wanafunzi hao-

WANAFUNZI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA

     Akifungua warsa hiyo Mwenyekiti wa SEPSSA Sande Salum, ambaye ni mwanafunzi wa Shahada ya Elimu Maalumu, Sayansi ya Siasa na Uongozi (POLITICAL SCIENCE NAD PUBLIC ADMINSTRATION) aliwasihi wanafunzi hao kuzielewa haki zao za kimsingi pamoja na kuwajibika kwa faida yao na Taifa kwa ujumla, Huku akiwaelezea umuhimu wa Rasilimali zilizoko wilayani kwako ikiwa ni pamoja na misitu na mazao mbalimbali ya chakula na matunda pia.

MWENYEKITI WA SEPSSA AKIWASILISHA MADA

Mwenyekiti huyo alieleza kuwa watatoa Elimu ya Uraia kwa Shule zote za msingi na Sekondary, pamoja na kwa Wananchi wote kwa ujumla, hii ni kutokana na wanachi wengi hasa wa vijini kutokuwa na Elimu ya uraia na hivyo kupelekea kuchagua viongozi wazembe na wasio wawajibikaji, na hivyo kurudisha maendeleo ya jamii nyuma na Taifa kwa ujumla.

MHAMASISHAJI TEDDY SANGA AUGUSTINO

KUTOKA KUSHOTO, HEADMASTER WA MAGAMBA SECONDARY. 2, MWALIMU 3. MJUMBE WA SEPSS, SANGA TEDDY AUGUSTINO, 3. MWENYEKITI WA SEPSSA MR. SANDE SALUM




                  "SEPSSA FOR CHANGE"

Monday, August 1, 2011

kitabu " UKOMBOZI WA PILI WA TAIFA LETU" mtunzi, DEOGRATIUS KISANDU kipo mtaani.



     DEOGRATIUS PIO KISANDU, Ambaye ndie mtunzi wa kitabu hiki Ni mwanafunzi wa shahada ya elimu maalumu, siasa na uongozi katika chuo kikuu cha SEBASTIAN KOLOWA UNIVERSITY COLLEGE, TANGA'
    Ni katibu wa baraza la vijana wa chadema (BAVICHA) mkoa wa Tanga, pia aliwahi kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Lushoto kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA uchaguzi mkuu mwaka 2010.

DEOGRATIUS KISANDU, MWANDISHI WA KITABU.

 UKOMBOZI WA PILI WA TAIFA LETU,  ni kitabu kinachozungumzia ukombozi wa wananchi wa Tanzania kutoka katika ukoloni, Pia kwa upande mwingine kinazungumzia ukombozi wa watanzani walio wengi kutoka kwa watanzania wenzao walio wachache ambao wanatumia ufisadi ili wafaidi wao na familia zao.
  Kitabu hiki kinaamsha hamasa miongoni mwa wanaharakati wanaopenda haki na usawa, Wanaharakati wasiopenda rushwa, uonevu na ukandamizaji wa aina yoyote kutoka kwa mafisadi wachache.
  KITABU HIKI NI MAALUMU KWA WAPIGANIAJI HAKI KWA WANYONGE, WANAHARAKATI WASIOTISHIWA NA MITUTU YA BUNDUKI KATIKA KUDAI HAKI ZAO

JALADA LA KITABU
UZINDUZI WA KITABU KWA MKOA TANGA UTAFANYIKA SIKU YA ALHAMISI TAREHE 3/08/2011.  LAL HOTEL ( ofisi ndogo ya chadema) barabara ya 13 kwa 14 karibu na TANGA CINEMA ( majani ya chai) maeneo ya stend.NA KITAENDELEA KUZINDULIWA KATIKA MIKOA YOTE TANZANIA, TAARIFA YA WAPI NA LINI MTAIPATA HAPAHAPA.


    
kwa mawasiliano zaidi ya jinsi ya kupata kitabu hiki, piga simu no, 0655025609
                                                                                                     0786025609
                                                                                         kisandudp@yahoo.com


RIDER_DECEMBER OFFICIAL VIDEO, VIDEO DIRECTED BY TUMSIFU KOMBE THE GREAT

CHAZ MAVOKO-SONG KWAHERI, Video directed by Tumsifu the great films

wibiya widget

TUMSIFU THE GREAT © 2012.All Rights Reserved.Designed by Tumsifu Kombe Modified by Nicolaus Trac-0716 276 000 :ICT EXPERT Sponsored by: JIPANGE