MKASA WA KUSIKITISHA wa baba kumuua mwanae kwa kumzika akiwa hai kutokana na mgogoro wa
ndoa, umezidi kuibua mapya, baada ya mama mzazi wa marehemu ,Debora
Riziki (3), kusimulia mkasa mzima .
Akizungumza kwa hisia kali, kijijini kwake Ibula, katika kata ya Kiwira, wilayani Rungwe, Mama mzazi
wa Marehemu, Esther Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea
kulikuwa na viashiria vingi vya mumewe kufanya ukatili.
Alisema tukio la mzazi mwenza huyo kumwiba mtoto na kwenda kumfanyia
ukatili huo wa kinyama lilikuwa la pili, baada ya awali kumuiba akiwa na
miaka miwili na miezi mine na alimrudisha kwa maandishi ya serikali ya
kijiji.
Alisema katika tukio la kwanza la mtalaka wake huyo kumuiba mtoto wao
huyo, lilitokea Septemba mwaka 2012, baada ya wiki chache za kumfukuza
katika nyumba waliyokuwa wakiishi katika kitongoji cha Iponjola, kijiji
cha Asenga, nyumba iliyotumika kuzikwa mtoto huyo.
 |
| MAITI YA DEBORA |
Alitaja sababu za yeye kufukuzwa ni ugomvi uliotokana na yeye kuhoji
sababu za kuficha fedha kiasi cha sh. 120,000 zilizotokana na wao kwa
pamoja kufanya kazi ya kibarua katika mashamba kijijini hapo na baada ya
malipo kutolewa mtalaka wake huyo alionesha kiasi kidogo cha sh.80,000.
Alisema ugomvi huo ndio ulisababisha yeye arudishwe kwa wazazi wake,
lakini baada ya muda mfupi mwanaume huyo alimfuata na kumbembeleza ili
warudiane na alipogoma aling’ang’ania aondoke na mtoto .
“Nakumbuka ilikuwa Novemba mwaka jana baada ya mimi kuondoka nyumbani
kwake na kurudi kuishi hapa nyumbani, siku hiyo tukiwa shambani huyo
bwana alikuja hapa nyumbani na kumkuta mwanangu wa kwanza (Neema Steven )
niliyezaa na mwanaume mwingine” alisema Mwambenja.
Alisema baada ya kufika eneo hilo majira ya saa mbili asubuhi alitumia
ujanja na kufanikiwa kumuiba mtoto na kisha kutokomea naye kijijini kwao
Asenga, hali ambayo ilisababisha kutoa taarifa kituo cha polisi Kiwira.
“Unajua kuwa baada ya kwenda kutoa taarifa polisi walitusaidia kufika
kijijini kwao ambapo serikali ya kijiji ilikubali nimchukue mwanangu kwa
kuwekeana mkataba wa kisheria kwa mujibu wa sheria, kwani alikuwa chini
ya miaka saba”.
Aliongeza kuwa Novemba 15 mwaka 2012 serikali ya kijiji chini ya
Mwenyekiti, Lutengano Mwakyoma na mashahidi watano wakiwemo wazazi na
ndugu zake, walinikabidhi barua ya kuridhia kuondoka na mwanangu, huku
ikimuonya mume wangu kutorudia kosa hili la kumuiba mtoto hadi hapo
atakafikisha miaka saba.
 |
| MTOTO DEBORA ENZI ZA UHAI WAKE |
Tukio la pili la kuiba mtoto.
Alisema tukio hilo lilitokea Novemba 29 mwaka jana 2012, ambapo alifika
nyumbani kwao majira ya saa 12 :00 na kumkuta dada wa marehemu kumchukua
mtoto akimdanga kuwa anaenda kusenya kuni eneo la jirani.
Aliongeza kuwa baada ya kuona dada wa marehemu anang’ang’ania kwenda
wote alimuamuru arudi nyumbani kuchochea moto kwa kuwa kulikuwa
kumeinjikwa mboga na kukubali kurudi.
“kwa mujibu wa maelezo ya mwanangu huyu wa kwanza alisema baada kurudi
toka ndani, alikuta baba yake huyo ameondoka na mtoto na tuliporudi na
kupokea taarifa hizo tulichanganyikiwa na kuanza kuhangaika hovyo”
alisema mama wa marehemu.
Mwambenja alisema kuwa baada ya kucha siku ya pili asubuhi yake